Dar/Mikoani. Katika kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) vimegawana maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano
ya hadhara na mafunzo kwa viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati
wa ushindi.
Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF.
Chadema kilianza ziara zake mikoani wiki
zilizopita baada ya kuzindua mkakati wake uitwao ‘Hakuna kulala, Hakuna
kula, Mpaka Kieleweke’ nchi nzima wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka
kambi mkoani Kigoma kwa kile ilichokiita kuimarisha majimbo ya
kimkakati.
Sanjari na vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia
katika moja ya ngome zake, mkoani Mtwara pamoja na mipango mengine ya
kiushindi, kinahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.
Jitihada za Ukawa kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa
ni majuma kadhaa tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu
Mkuu wake Abdulrahman Kinana kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
Pia, ziara hizo ziligongana na zile za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho kipya kugongana Butiama.
Mimi nawaunga mkono UKAWA kwa juhudi na mpango wao wa kuungana.Katika dunia ya sasa viongozi/watu wanaungana kwa masirahi ya kuijenga nchi yao,pamoja na kufungua milango ya kidemokrasia ili kila mtu mwenye uwezo aweze kushiriki katika uongozi au nafasi ya kulitumikia taifa lake.Kwa mifumo ya demokrasia tuliyonayo hairuhusu kabisa kila mtanzania kushiriki kirahisi katika uongozi wa nchi hii.Ukiangalia hasa katika kipindi cha chama kimoja, mgombea mmoja na upande mwingi hakuna mtu wa kushindana naye.sio kwamba kulikuwa hakuna watanzania wenye uwezo wa kuongoza nchi.Ukiangalia staili hii bado ipo ndani ya CCM, watu wengine wamekatwa majina yao hata hawapewi muda wa kujieleza.Pengine wangejieleza matokeo yangekuwa tofauti.
ReplyDeleteUkiangalia demokrasia za wenzetu walioendelea wanaangalia uwezo wa mtu wa kulitumika taifa lake wala si anatoka chama gani.Kwa hiyo tunao watu wenye uwezo mkubwa lakini nafasi za kutumika hakuna zimeshikiliwa na watu wachache wakisema ndiyo ni ndiyo hapana ni hapana.