Mifuko hii
huwawezesha wawekezaji kuweka akiba na kuwekeza fedha zao na zikakua
zaidi.Hatimaye huwawezesha kufanya uwekezaji zaidi katika shughuli za
ujasiriamali,kupeleka watoto shule au kufanya shughuli zozote za kiuchumi.
Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko
mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko
wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye zaidi ya thamani ya Shilingi bilioni 235.
Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety,
Liquidity and Returns). Wawekezaji
wote wananufaika kwa kupata faida
shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu
wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya
vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
Ofisa
Masoko na Uhusiano UTT AMIS, Rahim Mwanga, akitoa maelezo kuhusiana na
mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS kwa Waziri wa
Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia (kushoto) na
Naibu Waziri TAMISEMI, Aggrey Mwanri wakati wa Mkutano Mkuu wa 31 wa
ALAT.
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akisaini kitabu cha wageni katika banda la UTT AMIS.
Naibu Waziri wa Elimu, Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni.
Mmoja
wa watu waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 31 wa ALAT akipata maelezo
kuhusiana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja kutoka kwa Ofisa Masoko na
Uhusiano UTT AMIS, Rahim Mwanga. Katikati ni Ofisa wa UTT AMIS, Waziri
Ramadhani.





No comments:
Post a Comment