KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 5, 2015

ANDIKISHENI WATOTO WAWEZE KUPATA VYETI VYA KUZALIWA - RITA

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. WAKALA wa usajili ufilisi na udhamini(RITA) wamewataka wazazi na walezi wanaosoma shule za msingi za Manispaa ya Kinondoni wawaandikishe watoto wao ili waweze kupata vyeti vyao vya kuzaliwa.

Hayo yamesemwa na Meneja masoko Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa RITA Josephat Kimaro  wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.

Kimaro amesema kuwa wananchi wajue umhimu wa cheti cha kuzaliwa kwani Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka inayodhibitisha taarifa muhimu za wananchi ikiwa ni pamoja na  tarehe ya kuzaliwa, mahali alipozaliwa, wazazi halisi na miliki halali wa cheti.

Pia Kimaro amesema kuwa  kila shule ya msingi ya Manispaa ya Kinondoni wameteua Mwalimu mmoja  ili kuhakikisha kila Mwanafunzi anapewa cheti cha kuzaliwa.

Amesema kuwa zoezi la uandikishaji  wa wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa ya Kinondoni, walioomba na waliopewa vyeti katika shule hizo ni wanafunzi 5081 kati ya hao ni wasichana 2720 na wavulana 2361.
 Meneja masoko Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa RITA Josephat Kimaro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Msajili wa vizazi na vifo Mariam Ling'ande.
Msajili wa vizazi na vifo Mariam Ling'ande akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Meneja masoko Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa RITA Josephat Kimaro
 Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na
Wakala wa usajili ufilisi na udhamini(RITA) jijini Dar es Salaam leo.(PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

.

No comments:

Post a Comment