KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 27, 2015

BREAKING NEWS:MAOFISA WA JUU WA FIFA WADAKWA NA MAREKANI KWA UFISADI

 
 Idara ya Sheria nchini Marekani zinapanga kuwashitaki maofisa wa FIFA kwa makosa ya ufisadi.

tayari maofisa wapatao 14 wameshatiwa nguvuni na wanatarajiwa kufikishwa mahakani kesho jijini New york. 

Maofisa hao wa FIFA wametiwa nguvuni usiku wa kuamkoa leo mjini  Zurich, ambako mkutano mkuu wa FIFA utafanyika Ijumaa na unatarajiwa kumpa Sepp Blatter awamu ya awamu ya tano ya uongozi.

Blatter achunguzwa

Blatter hajashitakiwa, maofisa wanasema, lakini ni miongoni mwa wanaochnguzwa na  maofisa wanasema uchunguzi huo unaendelea.

Maofisa walioko madarakani na walio karibu na Blatter, wanatarajiwa kuwa miongoni mwa watakao kabili mashitaka.

Mashitaka hayo ni sehemu ya uchunguzi wa FBI.

Uchunguzi wa mwanzo

FIFA imekuwa ndani ya uchunguzi wa rushwa kwa miaka kadhaa, lakini taasisi hiyo imekuwa ikikanusha madai hayo yanayowahusisha viongozi wake wakuu.

Mwezi wa Desemba, Kamati ya Maadili ya FIFA ilisema ilikuwa inakamilisha uchunguzi wake wa madai ya rushwa katika kinyang'anyiro cha wenyeji wa kombe la Dunia kwa mwaka 2018 na 2022 nchini Urusi na Qatar.

Kamati ilisema kuwa uchunguzi wake ulibaini kwamba hakuna ushahidi wa rushwa hivyo kulikuwa hakuna ulazima wa kufanya upya zoezi la wenyeji wa kinyang'anyiro hicho.

Lakini FBI hawakukubalina na uchunguzi huo wa kamati ya FIFA.

Uchunguzi wa Marekani ulianza  baada ya aliyekuwa Mwendesha mashitaka wa marekani, Michael Garcia, aliyekodishwa na FIFA kuchunguza madai mbalimbali ndani ya FIFA kudai kuwa ndani ya taasisi hiyo kulikuwa na rushwa.

Mwaka 2011, walimpiga marufuku maisha Mohamed bin Hammam, mwanachama wake kutoka Qatar kujihusisha na soka kwa madai ya kukiuka maadili.

Mashitaka kufanyika Marekani
Kinachotakiwa kwa mamlaka za sheria za Marekani kuwezesha kesi hizo kufanyika nchini Marekani.

Hata hivyo mamlaka za Marekani zinadai kuwa zinaweza kuwa na nguvu hiyo ya kisheria kuenedsha mashitaka hayo nchini mwao kutokana na haki za kisheria za matangazo ya televisheni yanayolipiwa mabilioni ya fedha wakati wa kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment