KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 4, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA TAMASHA LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA KATIKA SHULE YA SEKONDARI WAMA NAKAYAMA

9733
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akimpokea Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari Nyamisati iliyoko wilayani Rufiji kwa helicopter tarehe 2.5.2015. Mama Salma alikwenda Rufiji kwenye tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana katika Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ambayo inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo Mkuu wa Mkoa wa Pwani alikuwa Mgeni Rasmi.
9847
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kutoa hutuba yake wakati wa tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika kwenye Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama na kushirikisha pia Shule za Mahege na Nyamisati.
9876
Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika shuleni hapo tarehe 2.5.2015.
9887
Mtoa mada kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akieleza umuhimu wa wanafunzi kufundishwa Stadi za Maisha ili wanafunzi wa kike waweze kutimiza ndoto zao za maisha.                                              

No comments:

Post a Comment