
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko na majonzi
makubwa kifo cha aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari mahiri na
mhariri wa gazeti la mtandaoni, Mwanahalisi Online, Edson Kamukara,
kilichotokea ghafla jana jioni katika mazingira yanayodaiwa kuwa ni
ajali ya moto.
Kumwelezea
Edson Kamukara ambaye kabla ya kuhamia Mwanahalisi Online
linalomilikiwa na Hali Halisi Publishers, alikuwa Mhariri wa Gazeti la
Tanzania Daima, akiwa ametokea Gazeti la Jambo Leo ambalo alijiunga nalo
akitokea Gazeti la Majira, katika nafasi hii ya salaam za pole yenye
ukurasa mmoja, linaweza kuwa jambo gumu sana.
Marehemu
Kamukara alikuwa mmoja wa waandishi makini na mahiri ambao tasnia ya
habari ingeweza kujivunia kuwa nao (wakiwa hai) kwa muda mrefu, hususan
katika changamoto kadhaa ambayo taaluma hiyo adhimu inapitia kwa sasa
nchini Tanzania.


No comments:
Post a Comment