![]() |
Aliko Dangote
Mtu tajiri barani Afrika Aliko
Dangote amesema kuwa bado anataka kuinunua kilabu ya Arsenal licha ya
kushindwa kufanya hivyo mwaka 2010 alipotaka kununua hisa za kilabu
hiyo.
Bilionea huyo kutoka Nigeria ni tajiri mara nane ya
alivyokuwa wakati alipojaribu kununua hisa za klabu hiyo na kwamba
shabiki huyo wa Arsenal bado hajatupilia mbali ndoto yake ya kutaka
kuinunua kilabu hiyo ya Landon Kazkazini.
''Bado nina matumaini
kwamba siku moja nitainunua timu hiyo',' alisema Dangote mwenye umri wa
miaka 58.''Naweza kuinunua bei ambayo wamiliki wake itakua vigumu
kukataa'', huku akiongezea kuwa ''najua mpango wangu''.
La kushangaza ni kwamba Dangote ametaja hadharani kwamba Arsene
Wenger anafaa kubadilisha mbinu yake akisema kuwa timu hiyo inahitaji
mwelekeo mpya.
Dangote ambaye ana thamani ya dola bilioni 15 ni
tajiri zaidi ya Stan Kroenke ambaye anamiliki hisa nyingi katika kilabu
hiyo na Bilionea raia wa Uzbek Alisher Usmanov ambao wamekuwa
wakipigania udhibiti wa kilabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni.
|
June 22, 2015
DANGOTE:BADO NINA KIU YA KUINUNUA ARSENAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment