KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 18, 2015

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA SIKOSELI DUNIANI

Displaying 01.JPG
Mtoto anayeugua ugonjwa wa Sikoseli, Nasma Khalid (wa pili kushoto), akikikata keki wakati wa utambulisho wa Maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam leo. Wanaongalia kutoka kushoto mstari wa nyuma ni; Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya  Damu ya MNH, Dk. Stella Rwezaura, Mratibu wa Tiba na Tafiti, Dk. Furahini Chinenere, Mratibu wa Upimaji Sikoseli kwa Watoto, Dk. Deogratius Soka na baadhi ya watoto wanaougua sikoseli. Siku ya Sikoseli Duniani huadhimishwa Juni 19 kila mwaka.
Displaying 02.JPG
Mmoja ya watu wanaoishi na Sikoseli ambaye pia ni mwanzilishi wa asasi ya watu wanaoishi na ugoinjwa huo, Arafa Salim Saidi akitoa ushuhuda wake jinsi anavyoishi maisha ya kawaida licha ya kukabiliwa na tatizo hilo. 
Displaying 03.JPG
Muuguzi wa Hospitali ya Muhimbili, Rehema Nkingi (kushoto) akimpima  msukumo wa damu, Maria Juma,  mmoja wa watoto waliohudhuria hafla hiyo. 

Displaying 04.JPG
  Mtoto Suleiman Joshua (katikati) akichukuliwa kipimo cha damu na fundi sanifu wa Hospitali ya Muhimbili, Ignas Tadei katika hafla hiyo. Kushoto ni mama yake, Meresiana Abel.
Displaying 05.JPG
Baadhi ya watoto wanaougua sikoseli na kuhudhuria kliniki ya ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimsikiliza mmoja wa watu wanaoishi na sikoseli, Arafa Salim Saidi akiwasimulia hadithi za watoto wakati wa hafla hiyo. 

No comments:

Post a Comment