| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Katikati ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakia Bilal. Picha na OMR |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha marehemu Simba. Picha na OMR |
| Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha marehemu Simba. Picha na OMR |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki swala maalumu ya kuswalia Jeneza (halipo pichani) na baadhi ya viongozi wa kitaifa wakati wa kisomo maalumu kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumuombea marehemu. Picha na OMR |


No comments:
Post a Comment