![]() |
| Gervais Rufyikiri |
Mmoja wa Makamu wa Rais Burundi ameikimbia nchi yake baada ya kudai kutishwa kufuatia hatua yake ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza kuongeza muhula wa tatu
Burundi iko kwemye machafuko tangu Rais Nkurunziza alipotangaza kwania muhula wa tatu kwenye uchaguzi utaofanyika julai mwaka huu
Gervais Rufyikiri aliiambia France24 TV kwamba kuongeza muhula watatu sio katiba inavyoeleza
Msemaji wa serikali alikanusha kwamba Rufyikiri alitishiwa maisha
Kuna taarifa kuwa Spika Mhe. Pie Ntavyohanyuma amekimbilia Ubelgiji akidai kuwa ameenda kutibiwa naye alimpinga Rais kugombea muhula wa tatu
Wote wawili wana uraia wa Ubelgiji.
Maandamano ya kumpinga yalinza Bujumbura baada ya Nkurunziza kutangaza kwamba atagombea muhula wa tatu



No comments:
Post a Comment