![]() |
| Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, James Mbatia KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, James Mbatia, imesoma bajeti mbadala wa ile iliyowasilishwa na Serikali, huku ikiainisha masuala kadhaa ya kukuza uchumi na kupunguza utegemezi...Anaandika Mwandishi Wetu ... (endelea). Kwa mujibu wa Mbatia aliye Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, katika kipindi cha miezi minne ijayo kuanzia sasa, Serikali ya CCM ianze kujiandaa kisaikolojia kuondoka madarakani na kupiisha kwa amani serikali adilifu itakayoongozwa na UKAWA kuingia madarakani ili waweze kuwatumikia Watanzania. Akiwasilisha maoni ya upinzani leo kwa Bajeti ya 2015/16, Mbatia amesema “tunapendekeza kukusanya Sh. bilioni 19,695.2 ambapo mapato ya kodi na yasiyo ya kodi Sh. bilioni 18,847.1 (sawa na asilimia 20) ya Pato la Taifa.”(P.T) Aidha, mapato ya halmashauri ni asilimia 0.9 ya pato la Taifa sawa na Sh. bilioni 848.1. Amesema hiyo ni bajeti isiyo na mikopo ya kibiashara, hivyo inalenga kulipunguzia taifa mzigo wa madeni, tofauti na ile ya serikali yenye mikopo ya masharti ya kibiashara ya 10% na hivyo kuwaongezea wananchi mzigo wa madeni. “Bajeti inayoendelea kusisitiza umuhimu wa kuwalipa pensheni wazee wote nchini wenye umri wa miaka 60 na kuendelea wakati ile ya serikali iko kimya kabisa kuhusu malipo ya pensheni kwa wazee wote nchini, kwani bado inaendelea kufanya upembuzi yakinifu usioisha,”amesema. |
June 16, 2015
MBATIA AIBOMOA BAJETI 2015/2016,ASEMA NI BAJETI LIPUA LIPUA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment