![]() |
mimba za totoni na mimba za umri
mdogo ni madhara makubwa yanayopatikana kwa watoto wa kike ambazo
hupelekea kukosa haki zake za msingi pamoja na kuishi katika maisha ya
hatarishi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Kazi na Utumishi wa Umma Mhe Haroun Ali Suleiman kwa niaba ya
Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na watoto Bi
Zainab Omar Moh’d wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
huko katika Ofisi hiyo Mwanakwerekwe.
Amesema kisheria mtoto chini ya
miaka 18 ni kosa kumuozesha kufanya hivyo ni kumkosesha haki zake za
msingi kwani mtoto bado anahitaji uangalizi wa wazee kwa kupata haki
zake zote na kumlinda katika maisha yake.
“Madhara yanayopatikana kwa watoto
wa kike wanaopata ujauzito pamoja na ndoa za umri mdogo ni kukosa haki
zake za msingi, maisha yake kuwa hatarini kwa kujaribu kutoa ujauzito
huo kwa njia zisio za kitaalamu kutokana na kuogopa aibu au kuogopa
kufukuzwa majumbani na wazai wao”, amefahamisha Waziri Haroun.
Amefahamisha kuhsu madhara hayo ni
kutoka damu nyingi wakati wa kujifungua na kupelekea kupoteza maisha
pamoja madhara ya kukos elimu.
“Mara nyingi tumekuwa tukishuhudia
kuwa ndoa za utotoni hazidumu hususan akiolewa na mtu mzima sana kwani
mume huyo huona kuwa yeye ameoa tu na sio mlezi, kwani wakati huu mtoto
huyu nahitaji kulelewa, kuelekezwa na kupata utulivu lakini ameoa
hutajia mengi ambapo mtoto hana uelewa navyo na hatimae huamua kuachana
na kupelekea madhara zaidi”, ameeleza Waziri huyo.
Aidha amekemea kutokomeza vitendo
vya utelekeza wa watoto na udhalilishaji wa kijinsia ambavyo vinaendelea
kuathiri jamii hivyo ameitaka jamii kutoa ushirikiano na kukubali
kutoa ushahidi pale unapohitajika.
Waziri huyo ameeleza kuwa Wizara
imeanzisha kituo cha huduma za simu kwa watoto “Child Help Line
itakayotumiwa watoto, wanawake, vijana na jamii kwa jumla ambao wataweza
kuripoti matukio ya udhalilishaji kwa njia ya simu na pia kupata msaada
na ushauri nasaha ili kunusuru watoto na vitendo hivyo pamoja na
kuwaunganisha na huduma nyengine pale inapohitajika.
Hata hivyo Mhe. Waziri amesema
wizara anathamini juhudi na mshirikano ya Taasis za Kimataifa za
Serikali na zisizo za Kiserikali katika masuala mbali mbali ya maendeleo
ya watoto ambapo ujumbe wa mwaka hu ni “TOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI NA
NDOA ZA UMRI MDOGO”
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR



No comments:
Post a Comment