| Afisa Sheria wa NAOT, Bw. Frank Sina (kulia) akizungumza
katika mafunzo hayo.
Na Mwandishi wetu
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imeendesha mafunzo ya siku
moja ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria juu ya Ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
na jinsi ya kuitafsiri yanayofanyika katika Hoteli ya Den France jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad alisema kuwa
mafunzo yanalenga kuwapa ufahamu juu ya ripoti za ukaguzi ambazo Ofisi yake
inazitoa, na jinsi ya kuzitafsiri na kushughulikia masuala ya maadili
yanatokana na ripoti za ukaguzi.
Prof. Assad aliongeza kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa
kuzingatia Kifungu cha 27 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, 2008, kama
ilivyofanyiwa mabadiliko na Sheria ya Fedha Na. 10 ya mwaka 2010.
Kwa mujibu wa kifungu hiki, kinawataka wakaguzi
wanaofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
mara tu wanapobaini kuwepo kwa viashiria vya ulaghai/kugushi au rushwa
wanapokuwa wanafanya ukaguzi kutoa taarifa kwa CAG.
Kifungu kinaongeza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali akithibitisha kuwepo wa viashiria hivyo anapaswa mara moja
kuvitaarifu vyombo vya dola vya uchunguzi na nakala ya taarifa hiyo
kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.
“Kifungu hiki kinaeleza vyombo hivyo vya dola (DCI/PCCB)
kufanya uchunguzi wa kitaalamu juu ya tuhuma hizo na kukamilisha zoezi la
uchunguzi ndani ya siku 60 tangu siku ya kwanza. Mara baada ya kumaliza
uchunguzi huu vinapaswa kuwasilisha ripoti yao kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa
ajili ya maamuzi ya hatua za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa. Mkurugenzi wa
Mashitaka anapaswa kwa mujibu wa kifungu hiki kumtaarifu Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu juu ya hatua alizochukua,” Prof. Assad alifafanua.
|
| Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Bibi Felista Tirutangwa (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri yaliyofanyika katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam. |
| Washiriki wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri wakimsikiliza kwa makini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (aliyesimama). Mafunzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam. |


No comments:
Post a Comment