MSHAMBULIAJI
wa timu ya Stand
United,Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa habari mkoani
Tanga mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya
Coastal Union,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga
Mnigeria wa Stand, Abasarim
Chidiebele
MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand
United,Abasarim Chidiebele amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Coastal Union
kwa mkataba wa miaka mmoja katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara.
Chidiebele atua mkoani Tanga juzi
kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo
utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa
Coastal Union,Kassim El Siagi,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai na viongozi
wengine.
Akizungumza mara baada ya
kusaini,Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na
kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo
katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.
“Nashukuru kusajili Coastal Union kikubwa niwahaidi tu wapenzi,wanachama
na mashabiki kutumia uwezo wangu katika kuipa mafanikio timu yetu “Alisema
Mshambuliaji huyo ambaye ni tishio hapa nchini.
Kwa upande wake,Ofisa Habari wa
Klabu ya Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa msimu huu timu hiyo
imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaowawezesha kuhakikisha wanachukua
ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Unajua usajili wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani
hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua
Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao “Alisema.
Hata hivyo aliwataka wapenzi
mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha kufanikisha malengo
yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa kuanza kufanya vizuri katika
michuano ya Ligi kuu.
Mwisho.
0714543839
|
June 18, 2015
PICHA ZA CHIDIEBELE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA KUITUMIKIA COASTAL UNION
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment