Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis
kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika
siku ya jumamosi nchini humo.
Mchezo huo wa marudiano kuwania
kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa
siku ya jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia majira
ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kocha mkuu wa Taifa
Stars Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kinaendelea vizuri
na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini
Uganda.
“Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi,
vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya
vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisem Mkwasa.
Taifa
Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi jioni kwa usafiri wa
shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji
20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.
Aidha Mkwasa amesema
ataongea na waandishi wa habari siku ya alhamis asubuhi saa 5 kamili -
Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa
marudiano na kuweka wazi kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Uganda.
Stars
imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya
mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya
saa 10 jioni.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment