Pamoja na ahadi hiyo, amesema hawezi kutoa jibu lolote kwa
sasa kama atagombea tena au hatagombea ubunge katika jimbo lake la Bunda kwani
haijaingia katika kinyang’anyiro hicho cha urais kwa ajili ya kushindwa.
Akizungumza na wanahabari kabla ya kukutana na wadhamini
wake zaidi ya 100 waliojitokeza kumdhamini mjini Iringa jana, Wassira alisema;
“mimi ni mtu mwenye uzoefu mkubwa wa kuongoza Watanzania, kwa hiyo ninaamini
nina fursa kubwa zaidi ya kuwa mgombea.”
Akizungumzia idadi kubwa ya wanaCCM wenzake wanaojitokeza
kuwania nafasi hiyo ya juu, alisema hashangazwi hata kidogo kwani CCM ina
hazina ya viongozi wengi wenye sifa za urais japokuwa katika hao waliojitokeza
hakuna anayemhofia.
“Tofauti na wale wenzetu, wao wana mtu mmoja mmoja tu katika
vyama vyao, ukizungumza CUF utamtaja Lipumba (Ibrahim) na vyama vingine ni
vivyo hivyo; ni sasa tu baada ya kuunganisha vyama vyao kupitia umoja usio
rasmi angalau unaweza kuona kama wako wengi, lakini kiuhalisia ni wale wale
wanaotegemewa na vyama vyao,” alisema.
No comments:
Post a Comment