KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 7, 2015

BOSS MPYA WA MSD HUYU HAPA

5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Laurean Rugambwa Bwanakunu (pichani) kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD). Taarifa iliyotolewa Dar es salaam leo, Jumatatu, Julai 6, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Ndugu Bwanakunu unaanzia Juni 23, mwaka huu, 2015.
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bwanakunu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ariel Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiative.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Julai,2015

No comments:

Post a Comment