Mbunge wa
Kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR mh David Kafulila amezidi kuujengea
sifa Mkoa wa Kigoma na kuwa miongoni mwa wabunge na watu maarufu kutoka
mkoani Kigoma kufanya vizuri kitaifa, awali sifa za mkoa huo maarufu kwa
vipaji mbalimbali ilikuwa imeanza kutoweka kutokana na wanasiasa
wanaotokea mkoani humo kutuhumiwa kuwa wasaliti na kuvuruga ustawi wa
upinzani nchini kwa kudhaniwa wanatumiwa na chama tawala CCM ili
kuudhofisha upinzani nchini.
Mh
Kafulila ameyasema hayo leo jijini Dar-es-Salaam mara tu baada ya
kupokea tuzo ya mwanasiasa bora mwenye maono,(kiongozi mwenye maono)
Sambamba na Kafulila kupewa tuzo hiyo na taasisi ya Dream Success
Enterprises.
Wengine
waliopewa tuzo hiyo ni mwanahabari nguli wa habari za uchunguzi na
habari za kina Said Kubenea pamoja na mwanahabari pekee mwanamke
alionesha kupambana kwa vitendo dhidi ya vita ya mauaji ya Albino nchini
bi Vicky Mtetema, huku Kubenea akipewa tuzo ya uwazi na ukweli
No comments:
Post a Comment