KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 5, 2015

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, ZITTO KABWE WASHIRIKI KAMPENI MAALUM YA KUWACHANGIA WANAHABARI WANAOSUMBULIWA NA MAGONJWA SUGU

8
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Said Meck Sadick akisalimia na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe walipokutana katika kampeni ya kuosha magari ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.
2
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Said Meck Sadick akiongeza na washiriki katika tukio la kuchangia mfuko kwa ajili wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani ambapo aliipongeza kamati iliyoratibu shughuli hiyo kwa manufaa ya waandishi wa habari na kuwataka kuukuza umoja huo kwa manufaa ya wanahabari na umuhimu wa wanahabari katika jamii ya Kitanzania na Duniani kwa ujumla.Kulia ni Mwenyekiti wa Kampeni hiyo iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu Bw. Benjamin Thompson.   
5
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe akiosha gari kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.   
6
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiosha gari kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.  
7
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiosha gari kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.    

9
Baadhi ya wanahabari na Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali wakiwa katika picha ya pamoja katika kampeni ya kuosha magari ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.  

Picha na Hassan Silayo-Maelezo    

No comments:

Post a Comment