KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 4, 2015

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA MAONESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubua wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa ambapo aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa ya maonesho haya kutangaza bidhaa wanazozalisha na kuanzisha mashirikiano ya kibiashara baina ya makampuni, leo Jijini Dar es salaam.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania Bi. Jackline Maleko akimkabishi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi ya mshindi wa jumla wa Maonesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa NSSF Bi. Eunice Chiume,wakati wa Uzinduzi wa Maonesho hayo Leo Jijini Dar es Salaam.
4
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo ya namna mtambo maalum wa kukata nyasi unavyofanya kazi, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania Bi. Jackline Maleko.
5
Baadhi ya Viongozi wa mashirika na Tasisi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubua wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa.
Picha na Hassan Silayo

No comments:

Post a Comment