Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. |
……………………………………………………………………………..
Na Maryam Kidikona Miza Kona –Maelezo Zanzibar
Serikali imetakiwa kuanzisha
kitengo cha Idara ya Mikopo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ili
kuwaondosha usumbufu wananchi wanapotakata kurejesha fedha za mikopo
waliochukua.
Akizungumza na waandishi wa
habari Afisa wa Vyama vya Ushirika Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Faki Khamis
Makame Ofisini kwake Gamba amesema wanavikundi waliochukua mikopo kwa
ajili ya kuendeleza vikundi vyao wanapata usumbufu wakati wanapotaka
kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
“Kuna malalamiko kutoka Idara ya
Mikopo kuwa wanavikundi kutoka vijijini hawarejeshi mikopo kwa muda
uliopangwa, tatizo katika Mkoa huu hakuna kitengo cha Idara ya Mikopo
kwa ajili ya kukusanya mikopo hiyo hivyo inakuwa usumbufu kwa
wanavikundi kutumia gharama kubwa kuliko pesa wanazozirejesha,”
ameeleza Afisa huyo.
Alisema kutokana na tatizo hilo
inakuwa vigumu kurejesha mikopo yao kwa wakati na kuitaka Idara ya
mikopo kuweka mwakilishi wa kukusanya marejesho ya mikopo yao ndani ya
Wilaya hiyo.
Afisa huyo wa Vyama vya Ushirika
alifahamisha kuwa kuwepo kwa kitengo hicho Wilayani kutasaidia
kupatikana kwa urahisi huduma hiyo pamoja na kuondosha usumbufu uliopo
katika Mkoa wao.
Alieleza kuwa tatizo la usafiri
kwa wanavikundi ni changamoto kubwa inayorejesha nyuma maendeleo na
juhudi wanazochukua katika kujikwamua na umasikini ndani ya Mkoa huo.
Wakati huo huo Afisa huyo wa
Vyama vya Ushirika amewataka wanachma wa Vyama hivyo kufanya uchaguzi
ndani ya vyama vyao ili kupata viongozi waliobora wenye uwezo wa
kuviendeleza vikundi hivyo.
Amesema sula la kuwa na viongozi
wenye uwezo wa kuviendeleza vikundi vyao, maendeleo ya haraka yanaweza
kufikiwa kwa kipindi kifupi.
“Nawaomba wanaushirika mufanye
uchaguzi ili kupata viongozi wazuri watakaoweza kuhifadhi kumbukumbu na
kuweka vyema hisabu katika vyama vyenu,”Alisema Afisa Ushirika .
Amewapongeza akinamama wa Wilaya
hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kuanzisha na kujiunga na vyama vya
Ushirika ambavyo vimekuwa mkombozi kwao na kuachana na ile tabia
iliyozoelekea yakuwa tegemezi kwa waume zao.
No comments:
Post a Comment