Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar. |
Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao. |
Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. |
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA |
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo. |
Matembezi ya hisani kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya CCBRT
NA FRANCIS DANDE
RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana aliongoza matembezi ya hisani ya kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto waliopinda miguu.
Matembezi hayo yaliyodhaminiawa na Benki ya Afrika – Tanzania, lengo kuu
lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni ya ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa watoto 400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu nchini kote,ilikuyabadili maisha yao na kuwa ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Benki ya Afrika – Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria kurejesha kwa jamii kile inachopata kwa kuwa inaendesha shughuli zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu wa kuhimiza usaidizi katika suala hili jema, kwa kuwa CCBRT inatoahuduma kawa jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze kupata matibabu,” alisema Mwanaidi .
Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza:
“ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi chote cha kampeni hii. Maisha ya a mamia ya watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha ya watoto hao bila kupata msaada kutoka kwa washirika wetu wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.” |
No comments:
Post a Comment