KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

August 27, 2015

TAARIFA ZA KIMICHEZO TOKA TFF

 
STARS KUWAVAA LIBYA KESHO

Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku nne katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe, timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, kesho ijumaaa itacheza mchezo wa kirafiki wa mazoezi katika uwanja wa kwanza wa hoteli ya Kartepe.

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya ratiba ya Stars ambapo mchezo kocha wake atatumia kutazama maendeleo ya kikosi chake, kabla ya kurejea nyumbani tayari kupambana na Nigeria Septemba 05, mwaka huu katika mchezo wa kuwania kufuza kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Timu imeendelea na mazoezi leo mara moja baada ya kufanya mazoezi mfululizo asubuhi na jioni kwa siku tatu, ambapo leo wamefanya mepesi kujiandaa na mchezo huo dhidi y timu ya Taifa ya Libya inayonolewa na kocha Javier Clemence raia na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania, Atletico Madrid, Atletico Bilbao.

Akiongelea maendeleo ya kambi nchini Uturuki, kocha mkuu wa Stars, 
Charles Mkwasa amesema vijana wake wanaendelea vizuri na progam yao ya mazoezi, ambapo wachezaji wote wanafanya mazoezi kwa usikivu na umakini mkubwa kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.

“Wachezaji wote wapo katika hali nzuri kama unavyoona, wanajituma, wanafanya mazoezi kwa nguvu, na kutokana na kuwa mazingira mzuri ya kambi, kila moja anaonyesha uwezo binfasi wa kutaka kupata namba katika kikosi cha kwanza” alisema Mkwasa.

Stars itacheza na Libya mchezo huo majira ya saa 5 kamili asubuhi kwa saa za Uturuki katika uwanja wa kwanza wa hoteli Kartepe, mudaa huo umepangwa na wenyeji kutokana na hali ya hewa itakayokuwepo siku ya ijumaaa.

Abdi Banda ni mchezaji pekee aliye majeruhi kwa sasa katika wachezaji waliopo kambini nchini Uturuki kufutaia kupata tatizo la kuchanika nyama za paja, na kwa mujibu wa daktari wa timu Dr, Yomba anapaswa kupumzika kwa takribani siku 10 kabla ya kuanza mazoezi mepesi tena.



 U-15 YAJIFUA MOROGORO

Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kilichopo kambini mjini Morogoro, kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya Morogoro mwishoni mwa wiki.

U-15 inayonolewa na kocha Bakari Shime, imeingia kambini mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya vijana hao kukutana kila mwisho wa mwezi na kucheza michezo ya kirafiki na kombaini za mikoa kwa lengo la mwalimu kutazama uwezo wa vijana wake na kuongeza vijana wengi atakaowabaini katika michezo hiyo.

Ikiwa mkoani Morogogoro, timu hiyo ya vjiana itacheza michezo miwili na kombaini ya mkoa huo ya vijana wneye umri chini ya miaka 15 siku za jumamosi na jumapili kabla ya kuvunjwa kwa kambi yao sikuya jumatatu.

TFF iliandaa utaratibu wa timu hiyo ya vijana kucheza michezo ya kirafiki kila mwisho wa mwezi ndani ya nchi, kabla ya mwezi Disemba kwenda katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa.

Lengo la kambi hiyo ni kuandaa kikosi bora cha vijana kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wneye umri chini ya miaka 17 (U17) zitakazofanyika nchini Madagascar.


 TWIGA YAZIDI KUJIFUA ZANZIBAR

 Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars) inaendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar kujiandaa fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika mwezi ujao nchini Congo Brazzavile.

Twiga chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage imeendelea na mazoezi kisiwani humo kwa takribani mwezi mmoja sasa kujiandaa na fainali hizo abapo imepangwa kundi A na wenyeji Congo- Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

Mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya (Harambee Starlets) mwishoni mwa wiki iliypita, kocha wa Twiga Kaijage ameendelea kufanyia marekebisho yalitojitokeza katika mchezo huo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanakua vizuri kabla ya kuanza kwa fainali hizo.

Kikosi cha wachezaji 21 pamoja benchi la Ufundi na kiongozi wa msafaa wanatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Congo-Brazzavile tayari kwa kushiriki kwa fainali hizo za Michezo ya Afrika zitakazoanza kutimua vumbi Septemba 3- 19, 2015.

Katika hatua nyingine Shirikiksho la Mpira wa Miguu chini  (TFF) limewaomba wadau, wadhamini, taasisi na mashirika mbalimbali kujitokeza kuzidhamini timu za Taifa za vijana U15 na Twiga Stars.

Twiga Stars inayokwenda kushirki fainali za michezo ya Afrika inahudumiwa na TFF pekee, hivyo ni nafasi nzuri kwa mashirika, wafanyabiashara kujitokeza kuidhamini timu hiyo ya wanawake inayokwenda kupeperusha bendera ya nchi kwenye michuano hiyo.

Aidha timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 pia inahudimiwa na TFF pekee katika program ya kuandaa kikosi bora kitakachoshiriki kwenye kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika mwaka 2017.

TFF peke yake haina uwezo wa kuziandaa timu hizo, hivyo inawaomba wadhamini kujitokeza kudhamini timu hizo katika progam za mapinduzi ya mpira wa miguu nchini.
  
RATIBA YA FDL YATOKA

Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) imetoka  ambapo itaanza kutimua vumbi tarehe 19 Agosti, 2015 kwa timu 24 zinazoshiriki ligi hiyo kutoka katika mikoa mbali mbali nchini.

Ligi hiyo ya Daraja la kwanza inatarajiwa kumalizika Machi 12, 2016 ina makundi matatu yenye timu nane kwa kila kundi, kila kundi litacheza michezo saba nyumbani na ugenini na mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja kwenye Ligi Kuu ya Vodacom nchini.

Kundi A lina timu za African Lyon (Dar es salaam), Ashanti United (Dar es slaam), Friends Rangers (Dar es salaam), Kiluvya FC (Pwani), Polisi Dar (Dar es salaam), KMC FC (Dar es salaam), Mji Mkuu (Dodoma) na Polisi Dodoma (Dodoma).

Kundi B lina timu za Kurugenzi (Iringa), Burkinafaso (Morogoro), JKT Mlale (Ruvuma), Lipuli FC (Iringa), Ruvu Shooting (Pwani), Njombe Mji (Njombe), Kimondo  FC (Mbeya) na Polisi Moro (Morogoro).

Kundi C linaunda na timu za Panone FC (Kilimanjaro), JKT Oljoro (Arusha), Polisi Mara (Mara), Rhino Rangers (Tabora), Mbao FC (Mwanza), Polisi Tabora (Tabora), Geita Gold (Geita) na JKT Kanembwa (Kigoma).
  
TFF YAMPONGEZA BAYI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za pongezi kwa katibu mkuu wa TOC nchini Filbert Bayi kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF).

Katika salam zake Malinzi amempongeza Bayi kwa kuchaguliwa katika nafasi hiyo muhimu ya kutunga na kupitisha sheria zinazotumika katika michezo ya Olimpiki Duniani.

Bayi amechaguliwa katika nafasi hiyo ya Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Olimpiki dunanI katika uchaguzi uliofanyika nchini China, ambapo ataitumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne.

Kwa niaba ya famili ya mpira wa miguu nchini, TFF inamtakia kila la kheri FIilbert Bayi katika nafasi hiyo aliyochaguliwa na kuahidi kuendelea kushirkiana nae katika kuendeleza michezo nchini.


 MISRI YAJITOA ALL AFRICA GAMES

Nchi ya Misri imetangaza kujiondoa dakika za mwisho kushiriki kwenye fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) kwa timu zake za Wanawake na Wanaume, fainali zinazotarajiwa kuanza kutimu vumbi mwezi Septemba nchini Congo- Brazzavile.

Kwa mujibu wa kifungu cha 19 (B) cha uendeshaji wa michuano hiyo kinasema “Kama timu itajiondoa baada ya kuwa imeshafuzu kwa hatua ya fainali, lakini kabla ya kuanza kwa michezo yenyewe, Kamati ya Uendeshaji wa Mashindano itaziba nafasi hiyo kwa kuteua timu iliyotolewa katika hatua ya mwisho”.

Kujitoa kwa timu za wanawake na wanaume za Misri, kunatoa nafasi kwa Kamati ya Uendeshaji wa Mashindano kuzipa nafasi timu za Senegali (Wanawake), na Burundi (Wanaume) ambazo zilitolewa na Misri katika hatua ya mwisho.

Misri ilipangwa katika kundi B kwa Wanawake na timu za Cameroon, Ghana na Afrika Kusini, huku timu ya Wanaume ikiwa kundi B na timu za Ghana, Senegal na Nigeria

Wakati huo huo Mwamuzi Ferdinand Chacha kutoka Tanznaia ameteuliwa kuwa miongoni wa waamuzi wa michuano ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) nchini Congo-Brazzavile.

TFF inampongeza Chacha na kumtakia kila la kheri katika kuipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment