![]() |
| Justin Gatlin na Bolt wakipambana
Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt,
ameshinda medali yake ya pili ya dhahabu, katika mashindano ya riadha ya
dunia yanayoendelea mjini Beijing nchini Uchina.
Bolt alitimuka
mbio hizo kwa muda wa sekunde 19.55 na kunyakulia taifa lake medali
nyingine mbali na kuandikisha rekodi ya kuwa mwanariadha kasi zaidi
duniani katika mbio za masafa mafupi.Ushindi huo ni wa kumi kwa mwanariadha huyo kutoka Jamaica na ni ya nne mfululizo katika mbio hizo za dunia. Justin Gatlin wa Marekani, pia alishinda medali ya fedha katika mbio za mita mia moja, alimaliza wa pili akifuatwa na Gatlin alitumia sekunde 19.74. Katika fainali za mita mia nne kwa kina dada Felix Allyson wa Marekani alinyakuwa medali ya dhahabu, huku Shaunae Miller wa Bahamas akiridhika na medali ya fedha. Shericka Jackson wa Jamaica naye alizoa medali ya shaba kwa kutumia muda wa sekunde 49.99. Bingwa wa dunia wa mbio mita mia nane kwa kina dada, Mkenya Eunice Sum, nusura ayaage mashindano hayo pale alipomaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za mchujo. |
August 28, 2015
USAIN BOLT BINGWA WA DUNIA MITA 200
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment