RPC
wa Mkoa wa Dodoma SACP. David A. Misime akiongea na waandishi wa Habari
leo akitoa tahadhari juu ya matapeli wanaowadanganya na kuwatapeli
wastaafu. LAPF kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
imefanikiwa kumkamata mtu mmoja na kumfikisha Mahakamani baada ya
kujifanya ni mtumishi wa TAMISEMI, LAPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA
YA AFYA na kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu
kutoka katika mikoa mbalimbali.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa ufafanuzi katika mkutano huo na waandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 02.09.2015
MFUKO wa Pensheni wa LAPF unapenda
kutoa kutoa tahadhari hasa kwa Wastaafu au wanaotarajia kustaafu,
Idara, Wizara zote zinazoshughulika na wastaafu, Wakurugenzi wa Manispaa
na Halmashauri kujihadhari na watu wanaowapigia simu na kujitambulisha
kuwa wao ni watumishi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii na Idara zingine
za Serikali na kwamba wanashughulika na mafao ya wastaafu.
LAPF
inatoa tahadhari hiyo kwa sababu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja kwa jina la DAVID MAGESA
MAKALI @ PETER MABULA na kumfikisha Mahakamani baada ya kujifanya ni
mtumishi wa TAMISEMI, LAPF na OFISI YA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA na
kufanikiwa kuwaibiwa fedha kwa njia ya mtandao wastaafu kutoka katika
mikoa mbalimbali.
Wanachofanya
watu hao wanapiga simu Idara mbalimbali na kujifanya wapo TAMISEMI au
Wizara nyingine na kuwataka wawatumie orodha ya wastaafu wa mwaka fulani
pamoja na namba zao za simu. Inaonyeha kwa njia hiyo wameweza kupata
orodha ya wastaafu takriban kutoka katika Mikoa 15 hususan kutoka Idara
ya afya.
Wakishapata
orodha ya majina ya wastaafu na namba zao za simu humpigia mstaafu na
kujitambulisha anatokea Wizarani na anashughulikia wastaafu ambao
inaonekana walipunjwa kwenye mafao yao na inaonyesha naye amepunjwa
kiasi cha milioni fulani.
No comments:
Post a Comment