KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 23, 2015

MGOMBEA MWENZA BI. SAMIA SULUHU AMNADI DK. MAGUFULI WILAYA ZA KOROGWE NA LUSHOTO

Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii na wananchi wengine alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi leo Mjini Korogwe ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga. Baadhi ya wasanii waigizaji, Wema Sepetu (kulia) na Bibi Mwenda wakizungumza na WanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kuwashawishi waichague CCM kutokana na mazuri mengi iliyowafanyia wasanii. Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (katikati) katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza uliofanyika Lushoto Jimbo la Mlalo. Kulia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi. Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza leo viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Profesa ‘Maji Marefu’ akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza uliofanyika Korogwe Mjini leo. Sehemu ya wanaCCM na wananchi Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Kwagunda, Salehe Abdullah (kushoto) akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM leo kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza na kukikimbia chama chake cha CHADEMA. Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza huku wakiendelea na biashara zao sokoni hapo. Sehemu ya wananchi  na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha njiani Mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (kushoto) akibadilishana jambo na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Lushoto, Balozi Abdul Mshangama leo katika Jimbo la Mlalo. Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Jimbo la Mlalo, Lushoto. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mlalo, Shaban Omar Shekilindi akizungumza na wapiga kura wake jimboni Mlalo. Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na umati katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Makamba akizungumza aliwaomba wananchi wasikipe kura chama cha Chadema na ushilika wao wa UKAWA kwani wapo kwa ajili ya mabadiliko ya nafsi zao na si vinginevyo. Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mlalo, Shaban Omar Shekilindi alipokuwa akizungumza na wapiga kura wake jimboni Mlalo.

No comments:

Post a Comment