![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana (kulia), akikabidhiwa zawadi ya kinyago. |
![]() |
| Hapa ni furaha tupu katika uzinduzi huo. |
………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya StarTimes Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vyombo vya Habari,
Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga ya Beijing wamezindua maonyesho
ya mfululizo wa filamu na tamthiliya mwaka 2015 ambayo yatajumuisha
filamu na tamthiliya za kusisimua za kichina barani Afrika.
Kuendelea
kwa kukua kwa muingiliano wa tamaduni baina ya watu wa Tanzania na
China kumefanya filamu na tamthiliya za China kwenye luninga zijizolee
umaarufu mkubwa na kuwa kichocheo kikubwa katika
kukuza mahusiano baina
ya nchi hizi mbili.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi.
Yang Peili amebainisha kuwa Tanzania itabaki kuwa mshirika wake mkubwa
na wataendelea kuimarisha mahusiano yao ya kitamaduni kupitia matangazo
ya maudhui ambayo yana nafasi ya kipekee kuwafikia watu wengi zaidi.
”Maonyesho
haya ambayo kwa kawaida yatakuwa ni ya filamu na tamthiliya kutoka
Beijing kwa kiasi kikubwa yataonyeshwa nchini Tanzania na Afrika kwa
ujumla. Kwa makadirio, jumla ya filamu na tamthiliya 30 za kwenye
luninga zitaonyeshwa nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
Dhumuni
kuu ni kuimarisha muunganiko wa maingiliano ya kiutamaduni baina ya
marafiki zetu wa Afrika na watu wa China.” Alisema Bi. Peili
Mamlaka
ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga itatoa
fursa ya kipekee kwa watazamaji wa barani Afrika kama vile Tanzania,
Kenya na Afrika ya Kusini kukutana na washiriki maarufu wa filamu
ya ‘The Young Doctor’. Pia wakurugenzi wa mamlaka hiyo watakuwa na wasaa
wa kuzungumza na kuyahoji makampuni ya kimataifa ya uzalishaji wa
vipindi barani Afrika kwa nchi hizo tatu.
Katika
miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ukuaji wa kasi wa tasnia ya filamu
na tamthiliya kwenye luninga na kunufaisha maisha ya watu huku masoko ya
tasnia hizo kwa nyumbani yakijulikana kimataifa na kuwa kiungo muhimu
katika kukuza muingiliano wa kiutamaduni baina ya nchi husika.
Kama
sehemu ya chombo cha uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za
Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015, sherehe za uzinduzi
zitafanyika nchini Afrika ya Kusini ambapo zitahudhuriwa na mamlaka ya
bodi hiyo ya Beijing.
“Maonyesho
haya yanafuatilia tukio kama hili ambalo lilifanyika mwaka jana na
kuandaliwa na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu
na Luninga ambapo Mr. Guo Jinlong, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mamlaka ya
Kisiasa ya CPC na Katibu wa Kamati ya Mamlaka ya Beijing alihudhuria
sherehe ya aina yake alipotembelea nchini Tanzania,” alisema Bi. Peili
na kumalizia, “Tamthiliya hizi za Kiingereza za kwenye luninga kama
zinavyojulikana miongoni mwa watazamaji wengi zimejizolea umaarufu
mkubwa burudani inayopendwa katika nchi nyingi za kiafrika na tunaamini
kwa pamoja tunaweza kuziunga mkono tasnia za uzalishaji wa vipindi za
nyumbani katika nchi husika ili kuweza kunufaika zaidi kwa pande zote
mbili.”
Uzinduzi
wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga
ya mwaka 2015 utajumuisha vipindi vya luninga maarufu na filamu kama
vile ‘The Young Doctor’, ‘The Sweet Burden’, ‘The Mi Family’s
Marriage’, ‘Ordinary World’, ‘Love is Not Blind’, ’20 Once Again’, ‘A
Wedding Invitation’, na ‘The Left Ear’ambazo zimepangwa kuonyeshwa
nchini Tanzania ndani ya kipindi cha mwaka mzima.
Shughuli
za kukuza maonyesho haya katika nchi zingine za barani Afrika zikiwemo
Kenya na Afrika ya Kusini zitafuatia kulingana na kampuni ya matangazo
ya dijitali ya StarTimes ambayo ina mpango wa kuzionyesha kupitia katika
ving’amuzi vyao vya antenna na madishi, na kwa uhaki.








No comments:
Post a Comment