![]() |
Mchungaji Mtikila Enzi za uhai wake |
![]() |
Mwanasiasa
maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji
Christopher Mtikila amefariki dunia kwa ajali ya Gari leo Majira ya saa
10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .
Taarifa
zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti
wa DP Mkoa Robart Kisinini wakati akizungumza na mtandao huu wa
www.matukiodaima.co.tz amesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa
amefariki dunia
RPC Pwani amesema ni kweli kuna ajali imetokea eneo la Msolwa ameenda kwenye eneo la tukio na atatoa taarifa baadae
Ajali
hiyo imetokea eneo la Msolwa mkoani Pwani huku Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Pwani akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa taarifa zaidi
ataitoa baada ya kurejea kutoka eneo la tukio. KWA HISANI YA .www.matukiodaima.co.tz
|
No comments:
Post a Comment