![]() | ||||
Mzee Kingunge Ngombale Mwilu(Pichani) amesema kuwa
hakubaliani na yaliyotokea mjini Dodoma wakati wa kumpitisha Dkt.Magufuli na
kilichotokea ni kuwadhalilisha wagombea. Alisema Kamati Kuu ilipaswa kuwahoji
"Hilo halikufanyika na wamewadhalilisha na kuwazungusha chini nzima
kutafuta wadhamini lakini hilo halikufanyika. Anasema Katiba ya CCM inasema
binadamu wote ni sawa na Binadamu wanastahili heshima" Kuwasumbua wazunguke na
kisha kuwafungia milango siyo kuwadhalilisha?"
Amesema kwa bahati mbaya hata viongozi hawajui haki zao na
hata wakizijua hawana ujasiri wa kuzitetea.
“Baadhi yetu tuliingia TANU si kwa kutafuta fedha au vyeo
..sisi wengine katika chama tulitafuta jambo lingine ,tulitafuta ukombozi wa
Waafrika,” alisema.
Uongozi wa sasa wa CCM umeamua kukibinafsisha Chama kwa
maslahi ya asiyejulikana mambo yanayofanyika ni ya ajabu.
Alisema vijana wanatumiwa kudhalilisha watu wazima,
mavuvuzela wanaajiriwa kuwatukana watu,na kwamba hicho si chama
walichoshirikiana kukijenga.
Alisema kuanzia leo anaachana na chama na kwamba hawezi
kukubali kuwa kenye chama kisichokubali fuata Katiba.
“Sasa nasema kuanzia sasa mimi najitoa kwenye chama cha
Mapinduzi,najua uamuzi wangu utawasubua baadhi ya ndugu zangu na jamaa zangu”
Anasema ameshiriki kukijenga na katika kuhakikisha kuwa
chama kinakuwa na demokrasia halafu chama kinavunja katiba.
Amesema kuwa hakusudii kujiunga na chama chochote,kwani amekuwa
mwanaharakati kwa miaka 61.
Amesema kuwa wananchi wengi hivi sasa wanataka mabadiliko,
anasema kuwa hata alivyokuwa Arusha wakati Mgombea wa Ukawa Edward Lowassa
anatangaza nia, alisema CCM lazima impe ridhaa mtu anayekubalika na wananchi
wengi.
Amesema kwamba kama kila mtu anataka mabadiliko lazima kuna
sababu.
“Hata mimi nataka mabadiliko,” alisema.
Alirejea historia ndefu ya namna nchi ilivyokuwa ndani ya
Chama kimoja na baadaye mfumo wa vyama vingi. Amesema tangu Rais Jakaya Kikwete achukue nchi uchumi umedumaa.
|
October 4, 2015
BREAKING NEWS:KINGUNGE AJITOA CCM, ASEMA CCM IMEISHIWA PUMZI YA KUONGOZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment