KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 7, 2015

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI AHAIDI WANANCHI WAKE KUWAJENGEA SOKO LA KISASA.

01
Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha mjini Silivestry Koka kupitia tiketi ya (CCM) wakati wa mikutano yake  ya  hadhara ya kampeni wakati akizungumza na wananchi wa maeneo mbali mbali katika kata mbali za visiga pamoja na kata ya Pangani.
02
Mgombea huyo ubunge jimbo la Kibaha mjini akiwa anawasili katika moja  ya mikutano yake huku akiwa anashangiliwa na umati wa  wananchi waliofika kumpokea kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
03
Wananchi wakiwa wanafuatilia jambo katika moja ya mikutano hiyo ya hadhara..
……………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo katika halmashauri ya mji wa Kibaha wameahidiwa kujengewa soka kubwa la kisasa  kwa ajili ya kuweza kuondokana na usumbufu waliokuwa wanaupata katika kufanya shughuli mbali mbali za  kuuza bidhaa zao lengo ikiwa ni kuwapa fursa kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko katika  kukuza uchumi.

Ahadi hiyo imetolewa na Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha mjini Silivestry Koka wakati wa mkutano mikutano yake  ya  hadhara ya kampeni wakati akizungumza na wananchi wa maeneo mbali mbali katika kata mbali za visiga pamoja na kata ya Pangani .

Koka  amesema kwamba endapo akichaguliwa na wananchi wake kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anaweka mpango mkakati kwa  kushirikiana na halmashauri ya mji ili kuweza kuwakomboa wafanyabiashara hao kwa kuwajengea soko la kisasa ambalo litaweza kuwasaidia kwa kisi kikubwa kuendeshea shguhuli zao za biashara.

Mgombea huyo alisema kwamba anatambua katika jimbo hilo kuna fursa nyingi za kiuchumi hivyo ujenzi huo wa soko pindi utakapokamilika utaweza utaweza kubadilisha hali ya kimaisha kwa wananchi hao kwani wataweza kubuni biashara mbali mbali ambazo watakuwa wanakwenda kuziuza sokoni hapo.
 
“Mimi kwa upande wangu napenda kuona wananhci wa jimbo la Kibaha wanapiga hatua kubwa katika suala zima la maendeleo, hivyo kitu amabcho nimeshajiwekea na nimeshaanza kukifanya ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo na soko kubwa la kisasa amablo litaweza kuwajumuisha wafanyabiashara mbali mbali wadogo pamoja na wale wakubwa lengo ni kukuza uchumumi,”
 
“Kuna vijana na wakinamama wengi wamekuwa wakipata usumbufu nah ii yote ni kutokana na kukutowa na eneo la kudumu amablo limetengwa kwa ajili ya kuendeshea kazi zao, hivyo mimi lengo langu kubwa pindi nikichaguliwa ni kuwawezesha kwa hali na mali wananchi wangu kwa kuwaongezea mitaji katika biashara zao ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea.
 
Pia Koka alisema kwamaba kwa sasa bidhaa amabzo zimekuwa zikitoka katika mikoa mingine zimekuwa zikipelekwa katika soko kuu ya Kariakoo, kitu ambacho alidai kuwa kinawezekana kwa jimbo la kibaha kuwa na soko lake ili bidhaa zote ziwe zinauzwa hapo na wananchi wataweza kuondokana na kero ya kwenda kujinunulia mahitaji yao katika eneo lingine.

No comments:

Post a Comment