Na
mwandishi wetu-Mtwara
Tatizo la watoto wa kike mkoani Mtwara kukatiza masomo
kutokana na sababu mbalimbali limepungua kwa
kiasi kikubwa baada ya uwepo wa mradi wa “Hakuna wasichoweza” unaoendeshwa na
T-Marc kwa ufadhili wa Vodacom Foundation.
Mradi huo umeonyesha mwelekeo wa kuweza kutatua
matatizo yanayowakabili watoto wa kike kutotimiza wajibu wao wa masomo
mashuleni, ikiwa ni pamoja na kutotimiza ndoto zao sambamba na kupunguza utoro.
Akizungumza wakati wakati wa mrejesho wa mwenendo wa
mradi huo kwa wadau wa elimu wa mkoa huu, Meneja wa Mradi huo, Doris Chalambo
alisema mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2013 kwa mkoa wa Mtwara ulilenga kufikia wanafunzi 10,200 wa
shule za msingi kuwapatia elimu ya afya, namna ya kujisitiri wakati wa hedhi na
kupatiwa vifaa vya kujisitiri ambapo katika thamini yake iliyotolewa chini ya
utekelezaji wake kwa mkoa wa Mtwara umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuweza kupunguza
tatizo la utoro.
“Lengo la mradi ni kufikia wasichana 10,200 kwa mkoa
wa Lindi na Mtwara lakini kwa mkoa wa Mtwara wanafunzi wapatao 7,077 tayari
wamefikiwa na tumekuwa tukiwapatia elimu juu ya hedhi, elimu itakayomsaidia
pindi anapokuwa kwenye hedhi afanye kitu gani pamoja na elimu ya afya na
madhara ya mimba za utotoni sambamba na kumsaidia vifaa vya kujisitiri (pedi)
na hii ni kutokana na kuwa suala la hedhi halizungumziwi kabisa katika jamii
yetu hivyo mtoto anapata changamoto na kumpelekea kukosa shule kati ya siku 2
hadi tano ndani ya mwezi mmoja na kumrudisha nyuma kieleimu,”alisema Chalambo.
Aidha alisema changamoto wanazokumbana nazo katika
kutekeleza mradi huo ni pamoja na baadhi ya shule kukosa miundombinu kama vyoo
na chumba maalumu kwaajili ya kusaidia wasichana katika masuala ya afya na kuwa, Mradi huo unatekelezwa kwa awamu
mbili ambapo awamu ya pili itakuwa mkoa wa Lindi.
“Katika kutekeleza mradi huu hatuwezi kufanikiwa bila
ya miundombinu, tumegundua shule nyingi vyoo sio vizuri, kwahiyo bila kuendana
na miundombinu sahihi hatuwezi kufanikiwa,”alisema Chalambo.
Akizungumza kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Mtwara,
Jose Kitenana alisema mradi huo umeweza kuleta mabadiliko katika mkoa huo na
kuwa serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha miundombinu ya shule
inakuwa rafiki.
“Mpango huu ni
mzuri na kwa sisi serikali hatuwezi kufanya kila jambo, hivyo kuna wadau
tunashirikiana nao kama T-Marc kutoa elimu ya afya kwa wanafunzi kwa udhamini
wa Vodacom Foundation ili kusaidia watoto wetu wa kike, na suala la miundombinu
bado zipo taratibu ambazo zinafanyika kuhakikisha wanajengewa mazingira
rafiki,”alisema Kitenana
Naye Mkuu wa Vodacom Foudation, Renatus Rwehikiza
alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwenye jamii katika vipengele
tofauti na sasa wanatekeleza mradi wa hakuna wasichoweza kwa lengo la kuongeza
mahudhurio ya watoto shuleni na kuwa itapunguza kasi ya magonjwa,utoro na mimba
za utotoni.
“Vodacom Foundation inatoa misaada kwenye jamii katika
vipengele tofauti na sasa hivi tuna mradi wa ‘hakuna wasichoweza’ umegharimu
kiasi cha 480 milioni ambao umetekelezwa kwa awamu na sasa kwa mkoa wa Mtwara
tumefikia ukingoni tunasubiri kupata tathmini ya huu mradi na awamu ya pili
tutakuwa mkoa wa Lindi lakini nina imani kwa kiasi kikubwa utasaidia kupunguza
ile kasi ya utoro na mimba za utotoni na kumwezesha mototo wa kike kutimiza
ndoto zake,”alisema Rwehikiza
Akizungumza mwanafunzi, Doreen Mvungi alisema mradi
huo umeweza kuwapa maarifa namna ya kukabiliana na changamoto walizokuwa
wakizipata pindi wanapopatwa na hedhi shuleni na kuondokana na aibu ya kuzomewa
waliyokuwa wakiipata toka kwa wavulana.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Chuno ya Mkoani Mtwara,wakiendelea na masomo yao baada ya kunufaika na mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi ili waendelee na masomo yao mashuleni.Mradi huo umedhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania. |
Meneja Mradi wa”Hakuna Wasichoweza” wa asasi ya T-Mark
Tanzania Doris Chalambo,akitoa tathmni ya mrejesho wa mradi huo kwa wadau
mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Mtwara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao
ulikuwa unaowapa
elimu ya hedhi na vifaa vya kustiwri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo
yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na
T-Mark Tanzania. |
Baadhi
ya wadau wa elimu wa Mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye warsha maalumu ya
mrejesho wa mradi wa”Hakuna wasichoweza”
unaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiri wasichana ili wasikose kuhudhuria
masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa
na T-Mark Tanzania. |
“Najivunia kuwa sehemu ya walionufaika na Mradi huu ni
mkombozi umetupa elimu ya afya, elimu namna ya kujisitiri tunapokuwa katika
hedhi na imewasaidia wengi kwani siku hizi hamna tena ile zomea zomea na hata
mahudhurio ya darasani yameanza kuwa mazuri kwa sisi wasichana tofauti na
zamani msichana alipokuwa akipatwa na ile hali anashindwa kujua nini cha
kufanya,”alisema Doreen
No comments:
Post a Comment