Mwenyekiti wa Kamati Taifa Stars, Farough Baghozah amewashukuru
watanzania kwa michango yao waliyoitoa kuispaoti timu ya Taifa ‘Taifa
Stars’ katika michezo ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini
Urusi dhidi ya Algeria.
Farough alianza kwa kuwashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi
katika mechi ya Taifa Stars na Algeria na kuwashukuru pia wale wote
waliosafiri na timu hiyo ya Taifa, Taifa Stars kwenda Algeria katika
mechi ya marudiano.
Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania, Makamu wa Raisi Mama Samiha Suluhu, Raisi Mstaafu
wa Awamu ya Nne, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani na viongozi
wote wa chama na serikali kwa njia moja au nyingine katika kusapoti timu
ya Taifa Taifa Stars kwenye Mchezo na Algeria
Naye Mkuu wa mkoa Dar es salaa, ambaye ni mlezi wa kamati hiyo, Mh
Mecky Sadick aliwashukuru watu wote, kuanzia wanakamati kwa jinsi
walivyojitoa kwa muda wao wote katika maandalizi na hasa kuhamasisha
watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ya taifa
kwa kuomnyesha uzalendo.
Kwa namna ya kipekee Mecky Sadick amewashukuru watu wote na makampuni
yaliyojitokeza katika kuchangia Timu ya taifa wakiwemo Jubilee
Insurance, Equity Bank, PPF, Serena Hotel, GSM, bila kusahau vyombo vote
vya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine waliweza kujitoa na
kuhamasisha watanzania wajitokeze kwa wingi uwanja wa taifa kuishangilia
timu yao.
Katika mchakato mzima wa awali wa mechi ya kufuzu kombe la dunia
2018, Kamati kupitia kwa wadau mbalimbali iliweza kuchangisha pesa jumla
ya milioni 122,640,000 za kitanzania, dola za kimarekani 19,800 na
177,000 kutoka tigo pesa na airtel money.
Matumizi ni dola za kimarekani 70355, na milioni 47,904, 743 za kitanzania.
Mwisho kamati imewashukuru sana Watanzania na na kuwaomba wadumishe umoja wtue.. Nchi Yangu, Timu Yangu Taifa langu.


No comments:
Post a Comment