Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
jijini Dar es Salaam, Bw.Injinia Thomas Haule, (katikati), akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa
uwanja huo leo Ijumaa Novemba 27, 2015. Utawala wa uwanja huo ulio chini
ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umejipanga upya katika
kuimarisha ulinzi ambapo kuanzia sasa, vifurushi na mizigo yote kutoka
posta itakaguliwa kwa mara ya pili kabla ya kupakiwa ndani ya ndege,
ikiwa ni hatua ya kudhibiti vifurushi na mizigo haramu kupenya kwenye
ndege. Kushoto ni Kaimu Meneja Usalama wa Uwanja huo, Bw.David Ngaragi,
(kushoto) na Afisa Usalama Mwandamizi wa Uwanja huo, Dorice Uhagile.
(Picha na K-Vis Media/Khalfan Said) |
No comments:
Post a Comment