Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa
Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach
Boys, Selemani Ally ‘Kaseja’ kibao cha namba za Pikipiki Dar es Salaam
leo.
Zungu
amesema ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa
kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa
mgombea Urais Dk John Pombe Mgufuli kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
ili iwasaidie kuongeza kipato.
Mbunge huyo aliendelea kusema ataendelea kusaidia maswala ya michezo ili
kuinua sekta hiyo kwa kusaidia vifaa vya michezo Zungu ameongeza na
kusema ” Leo nakusaidieni Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu,ya
wafanyabiashara wenyewe, na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye
maeneo mnayouzia samaki, Nitatekeleza hilo kabla ya mwezi wa kumi na
mbili ili mfanye biashara kwa uhuru.
|
November 30, 2015
MBUNGE WA JIMBO LA ILALA MUSSA ZUNGU ATEKELEZA AHADI ALIYOITOA WAKATI WA KAMPENI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment