Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Profesa Elisante Ole Gabriel leo amefunga program ya Live Your Goal
iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) katika uwanja
wa Karume jijini Dar es salaam. Ole Gabriel amewashukuru vijana waliojitokeza kushiriki katika program hiyo na kuwaomba wazazi kuwarushu watoto wa kike kujtokeza na kushiriki katika program hiyo ya kuhamasisha wanawake kucheza mpira wa miguu. Live Your Goal ni program inayoendeshwa na TFF kwa msaada kutoka FIFA yenye lengo la kuwahamasisha watoto wa kike, na wasichana kujitokeza kuucheza na kuupenda mpira wa miguu. Programu hii iliyomalizika leo imejumuisha vilabu sita vya wanawake, kutoka wilaya za Ilala, Kinodoni na Temeke, shule za msingi sita kutoka jijini Dar es salaam ambapo washiriki walikua wanafunzi wenye umri kaunzia miaka 8 na kuendelea, na ikifanyika kwa mara ya pili baada ya awalia mwezi Juni mwaka huu mkoani Geita. |
November 29, 2015
OLE GABRIEL AFUNGA LIVE YOUR GOAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment