KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 25, 2015

TOBAA! MSANII LINEX AGONGA GARI YA DC MAKONDA, NINI KILIMPATA? SOMA HAPA

DC Makonda
Msanii wa muziki wa Bongo Flava Sunday ‘Linex’ Mjeda, ameamua kuelezea mkasa uliomkuta baada ya ‘kuikwangua’ gari ya mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wiki tatu zilizopita.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook,Linex ameelezea hisani  aliyofanyiwa na Makonda licha ya kumfanyia makosa.
Usome ujumbe wake hapo chini then tuachie maoni yako.

“Katika mizunguko ya hapa na pale Kama week mbili tatu zilizo pita majira ya saa 9:00 usiku kwa bahati mbaya nilipiga pasi gari la mtu nikashuka kwa lengo LA kufanya makubaliano nae mara nikashangaa ameshuka mh @paulmakonda kwa kua sijawahi kukaa nae kokote wala kufahamiana nae nikajua Leo yamenifika lakini cha kushangaza aliposhuka

Aliangalia wapi pamekwaruzika then akaniambia ni bahati mbaya wakati mi nilijua atatumia nguvu au nafasi aliyo nayo serikalini kweli usiamini unachosikia au kuona hata chumvi saa nyingine hua Ina fanana na sukari ‪#‎TheVOA”  ameandika Linex.‬KWA HISANI YA MPEKUZI

No comments:

Post a Comment