| Marehemu
Willy Chiwango (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Mtendaji Mkuu wa
BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Mahmoud Zubeiry (kulia)
MWANDISHI nguli wa habari za michezo na burudani Tanzania, Willy Chiwango amefariki dunia.
Taarifa
kutoka kwa familia ya marehemu zinasema kwamba Willy Chiwango aliyewahi
kushinda tuzo ya Mwandishi Bora wa Michezo nchini amefariki usiku wa
kuamkia leo.
Na imeelezwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi, ambayo familia yake itatoa taarifa zaidi baadaye.
Hadi anakutwa na umauti, Chiwango alikuwa anafanya kazi magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo.
Lakini
enzi zake, marehemu alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari
nchini, ikiwemo shirika la IPP Media. Bwana ametoa, bwana ametwaa. Mungu
amfanyie wepesi huko alikotangulia, mbele yake, nyuma yetu. Buriani
Willy |
No comments:
Post a Comment