![]() |
Ziara inaendelea kiwandani hapo.
Akizungumza
katika kiwanda hicho, RC Makalla alisema kwamba amefurahishwa na hali
ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho, huku akiahidi kushirikiana
na uongozi wa Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje ya
nchi. Alisema atashirikiana na
serikali ya Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari hiyo ya nje, akiamini kuwa
kutasababisha kiwanda hicho kupiga hatua kwa kuuza sukari yao nchini |
![]() |
Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla akiwa kwenye ukaguzi wa kiwanda cha
sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani humo, kama sehemu ya kuangalia
hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. Picha na Mpigapicha
wetu.
Na Mwandishi
Wetu, Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa
Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara katika kiwanda cha Sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro ili kujionea hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. RC Makalla alijionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho sasa kinazalisha sukari tani 105,000 baada ya kubinafsishwa, tofauti na uzalishaji wa tani 35,000 tu hapo zamani. |
![]() |
“Kilio
cha kiwanda hiki ni uingizwaji wa sukari kutoka nje, hivyo Kilimanjaro
tutashirikiana kwa karibu na wenzetu wa Tanga ili kuweka ulinzi mkali
kwa ajili ya kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje kwa kupitia mkoani
Tanga.
“Naamini
tukifanya hivyo tutaweza kukiweka kiwanda hiki katika hali nzuri,
ukizingatia kuwa viwanda vyetu ili viweze kujiendesha vinapaswa kuuza
bidhaa zao vizuri na si kupata changamoto zinazoweza kuwaathiri kama
suala hili la sukari nyingi kuingia kutoka nje wakati wao pia ni
wazalishaji,” alisema Makalla.
Kwa
wiki kadhaa sasa RC Makalla amekuwa akifanya ziara mbalimbali mkoani
Kilimanjaro pamoja na kufanya vikao muhimu vyenye lengo la kuhakikisha
kwamba wanaenda mchaka mchaka ili kwenda sambamba na kauli ya hapa kazi
ya Dr John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|





No comments:
Post a Comment