Na Lorietha Laurence-Maelezo
Serikali imedhamiria kumalizia
deni la Makandarasi la kiasi cha zaidi ya bilioni 800 ifikapo Juni
mwaka huu ambapo tayari kiasi cha bilioni 400 zimeshalipwa katika
kufanikisha ujenzi wa barabara za ndani ya jiji la Dar es Salaam
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa wakati wa ziara yake
ya kukagua ujenzi wa barabara hizo leo jijini Dar es Salaam lengo ikiwa
ni kupunguza msongamano katika njia kuu.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha
kuwa inapunguza msongamano na hivyo kuwarahisishia wananchi wake
usafiri , kukamilika kwa ujenzi huo ni afueni kwa wakazi wa jiji la Dar
es Salaam” alisema Prof.Mbarawa.
Aliongeza kuwa ujenzi huo
umegharimu kiasi cha shilingi Tilioni 1.2 chini ya ufadhili wa serikali
yenyewe kwa asilimia 100 kupitia Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini
(RFB) .
Prof.Mbarawa aliongeza kuwa
kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi holela pamoja na
ulipwaji wa fidia na kuwaomba wananachi pale wanapofanya ujenzi kujenge
mbali na barabara ili kuepeukana na usumbufu wa mara kwa mara.
Naye Mkurugenzi Mkuu waWakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) Patrick Mfugale ameeleza kuwa tayari
baadhi ya wananchi wameshalipwa fidia kwa wale waliopisha ujenzi katika
maeneo ambayo barabara zinatakiwa kupita na hivyo kurahisisha
usafirishaji kwa wananchi wake.
“Natoa wito kwa wananchi kutoa
ushirikiano kwa kupisha maeneo yale yote yaliyowekewa alama kwa ajili ya
ujenzi ili kukamilisha ujenzi mapema iwezekanayo “ alisema Mfugale.
Ziara hiyo ya kukagua ujenzi wa
barabara za ndani ilianzia katika barabara ya Tanki Bovu kwenda Goba
kilomita 9.0,baadaye kuelekea ,Mbezi , Malambamawili,Kinyerezi hadi
Banana yenye urefu wa kilomita 14 na Tabata Dampo-Kigogo na ile ya
Ubungo Maziwa ,mabibo hadi External kilomita 2.25.
Maradi huo wa ujenzi wa barabara
za ndani upo katika awamu mbili huku awamu ya kwanza ya kilomita 27
ikiwa inatarajia kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na baadaye kumalizia
awamu ya pili ya kilomita 28 tayari kwa kuanza ujezni wa awamu ya tatu
barabara ya Goba-wazo hill kilomita 13.0,Mbezi Mwisho Malambamawili
–kifuru kilomita 6, na Goba –Makongo-Ardhi kilomita 9.
No comments:
Post a Comment