![]() |
Baadhi ya
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii
wakibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (katikati) wakati Kamati hiyo
ilipotembelea ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) jijini Dar es Salaam
Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeanza kutekeleza
mikakati mipya ya ukusanyaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa
wadaiwa ambayo itaongeza wastani wa ukusanyaji wa Tshs 2.6 bilioni za
sasa hadi kufikia Tshs 8 bilioni ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi ameyasema hayo (Jumatano,
Machi 30, 2016) jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea mbele ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyotembelea ofisi za Bodi hiyo
zilizopo Mwenge.
“Hadi
mwezi uliopita (Februari, 2016) tulikuwa tunakusanya wastani wa shilingi
bilioni 2.6 kwa mwezi, lakini sasa tumeongeza kasi na mikakati mipya
ambayo itawezesha kukusanya shilingi bilioni 6 mwezi Aprili na shilingi
bilioni 8 ifikapo mwezi Juni mwaka huu,” amesema Bw. Sabi aliyeteuliwa
kushika nafasi hiyo na miezi miwili iliyopita.
HESLB ilianzishwa ilianza kazi mwaka 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji na pia kukusanya mikopo kwa wanufaika.
Hadi
sasa, zaidi ya shilingi 2.1 trilioni zimetolewa kwa wanufaika na kati ya
fedha hizi, mikopo iliyoiva na inayopaswa kukusanywa ni shilingi 258
bilioni ambazo wanufaika wake wamemaliza au kusitisha masomo yao na
vilevile kumaliza muda wa kujipanga kuanza |
March 31, 2016
HESLB YAJIPANGA KUKUSANYA MADENI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment