![]() |
| Mgombea urais wa chama cha Republican
nchini Marekani Donald Trump amebadili msimamo wake muda mfupi baada ya
kusema wanawake wanaotoa mimba wanafaa kuadhibiwa, utoaji mimba
ukiharamishwa.Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC. Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali. Lakini muda muda mfupi baadaye, alibadili msimamo wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia wanawake kutoa mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa. Lakini hata baada ya kusema hivyo, alijitetea na kuongeza kuwa: “Msimamo wangu haujabadilika.” Mgombea huyo anayeongoza katika chama cha Republican anaunga mkono kupigwa marufuku kwa utoaji mimba, lakini kwa kutegemea hali. Utoaji mimba umekuwa halali nchini Marekani tangu 1973 kufuatia uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya Juu nchini humo. BBC |
March 31, 2016
TRUMP HANA MSIMAMO KUHUSU UTOAJI MIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment