
Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara 
Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia 
ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.
………………………………………
Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia 
watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.
Amevitaka
 vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo 
hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa 
kipato cha chini.
Mhe 
Ummy amewasili Mtwara jana akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. 
Mohammed Kambi ambapo alifanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya 
Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Amewaonya
 wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli 
na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma
 kwa kujichukulia sheria mkononi.

Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akizungumza na mmoja wa wazee aliyefika kupata matibabu katika Hospitali
 ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada kuwasili hospitalini hapo 
kuzungumza na wafanyakazi.

Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akizungumza na baadhi ya wananchi waliokusanyika nje ya hospitali 
kufuatia tukio la mwananchi kumpiga daktari.

Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyefika hospitalini 
hapo.

Mh. 
Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa 
wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na 
mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.

Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula wakimsikiliza Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).


No comments:
Post a Comment