![]() |
Miongoni mwa vurugu zilizotokea mji mkuu wa Bujumbura
Waziri wa
zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini
Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria.
Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni "mauaji".
Wafungwa
katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika
hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka
gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua.
Umoja wa
Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa
ikiyakanusha.BBC
|
March 31, 2016
WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment