JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Mchango wa Shilingi Milioni 10
kwa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili
kuchagia upanuzi wa kanisa hilo.
Fedha hizo zimekabidhiwa na Kaimu
Mnikulu Bw. Ngusa Samike katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya
pili ya Pasaka, iliyofanyika kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.
Kabla ya misa hiyo ya pili Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa pamoja na Waziri Mkuu
Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga,
walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia
shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao
unaendelea.
Katika Misa hiyo Paroko wa Parokia
ya Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia
kuadhimisha miaka 50 ya tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na
kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao
unachangiwa na waumini wenyewe.
Padre Mulinganisa amemshukuru Rais
Magufuli kwa mchango huo, na amemuahidi kuwa utatumika vizuri ili
uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na michango ya waumini wengine.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
03 April, 2016


No comments:
Post a Comment