Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli
amempigia simu mtangazaji wa kipindi cha Clouds360 cha CloudsTv,
Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa
Rais.
Rais amesema mshahara alioukuta na ambao analipwa ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000) na wala sio milioni 30 kama wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360.
Ameahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.
Gazeti la Nipashe toleo la leo lilikuwa na habari iliyowanukuu Tundu Lissu na Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .
Gazeti la Nipashe toleo la leo lilikuwa na habari iliyowanukuu Tundu Lissu na Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .
Hivi
karibuni, Dk. Magufuli ameahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo
inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa
zaidi usizidi kiasi hicho.
No comments:
Post a Comment