WABUNGE
wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, wametembelea
Clouds Media Group,Mikocheni jijini Dar es Salaam Aprili 22, 2016
ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya takriban siku 20 kutembelea vyombo vya
habari kwa nia ya kuvishirikisha vyombo hivyo kutoa elimu kwa wananchi
kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, inayomiliki kituo cha
radio, Clouds FM, Clouds TV, Bw. Ruge Mutahaba, amewaeleza wabunge hao
walioongozwa na mwenyekiti wao Mh. Chrles Makongoro Nyerere kuwa,
Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la kutogeuza vipaji kuwa biashara
na hivyo kujiingizia kipato.
Ruge
amewahimiza wabunge hao kushawishi serikali ya Tanzania kurekebisha
sera zake za kuwawezesha wananchi na kuwajengea uwezo wa kuvitumia
vipaji walivyojaaliwa na Mwenyezimungu ili kujiingizia kipato.
Akielezea
nia ya ziara hiyo, Mwenyekii Mh. Makongoro Nyerere alisema, wabunge
kutoka nchi wanachama walipewa jukumu la kuwatembelea wananchi wa nchi
watokako ili kwahimiza kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo
ambayo kwa sasa ina jumla ya wanachama sita, Tanzania, Kenya Uganda,
Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.
“Jumuiya
ya Afrika Mashariki ina soko la kutosha na wananchi wa Jumuiya hii
wanyo fursa ya kwenda kufanya shughuli za kiuchumi bila kizuizi chochote
ikiwemo biashara na kufanya kazi hivyo ni wakati wa watanzania kuacha
kulalamika na kuchangamkia fursa hiyo.” Alisema Mh. Makongoro.
Pamoja na Mh. Makongoro, wabunge wengine ni pamoja na Mh. Shy-Rose Bhanji, na Mh. Nderaikindo Kessy.
Imeandaliwa na K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Wabunge wa bunge la Afrika
Mashariki kutoka Tanzania, na wafanyakazi wa Clouds Media Group, akiwemo
mchekeshaji maarufu Bishanga Bashaija, wakiwa kwenye moja ya studio za
Clouds Media Group, wakati wa kipindi maarufu cha Leo Tena, Aprili 22,
2016.
Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group, Bw. Ruge Mutahaba, (kulia), akitoa
maelezo ya uendeshaji wa kampuni hiyo, wakati wabunge wa bunge la Afrika
Mashariki (EALA-Tanzania), walipotembelea studio za Clouds radio/TV
Mikocheni jijini Dar es Salaam Aprili 22, 2016. Kutoka kushoto ni
Mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere, Mh. Nderaikindo
Kessy, na Mh. Shy-Rose Bhanji.
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Gea Habib
Mwenyekiti Mh. Charles Makongozo Nyerere (kulia) akizungumza kwenye kipindi cha Leo tena
Mh. Shy-Rose Bhanji mkutanoni
Mh. Nderaikindo Kessy akiwa mkutanoni
Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena Husna Abdul “DAHUU”
Mwenyekiti Mh. Charles Mkongoro Nyerere akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana mawazo na uongozi wa Clouds Media Group.

Mh. Shy-Rose Bhanji, akizungumza kwenye kikao hicho
No comments:
Post a Comment