Wakazi
wa Mlandizi mkoa wa pwani na vitongoji vyake,Wamerahisishiwa jinsi ya
kupata huduma mbalimbali za huduma za mawasiliano
kwa kuzinduliwa kwa duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania
lililozinduliwa leo ukiwa ni mkakati uliowekwa na kampuni hiyo kwa
kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi nchini kote.Mwaka huu
kampuni hiyo imedhamiria kufungua vituo vipatavyo 500
nchini kote.
Kituo
hiki kipya kinatarajia kutoa huduma kwa wateja wa Vodacom wanaoishi
Mlandizi na vitongoji jirani ambao walikuwa wanatembea
mwendo mrefu kufuata huduma pia kitahudumia wasafiri mbalimbali
wanaotumia barabara ya morogoro .
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh amesema kuwa mkakati huu wa kufungua
vituo vya kutoa huduma za Vodacom umebuniwa ili kuwapunguza wateja adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma.
“Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka sehemu mbalimbali lakini bado
tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja wazipate popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
Aliongeza
kuwa kupitia huduma hii ya vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua
wigo wa ajira nchini kwa kuwa watanzania zaidi
ya 1000 watanufaika na mpango huu na ni utekelezaji wa moja ya
malengo ya kampuni ambayo ni kufanya uwekezaji wenye mwelekeo wa
kuwanufaisha watanzania.
Akifungua
kituo hicho kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Pwani, Kaimu Katibu tawala
wa Wilaya hiyo,Anathory Mhango aliipongeza
kampuni ya Vodacom kwa kusambaza huduma zake karibu na wateja na
aliwataka wakazi wa Mlandizi kutumia huduma za mawasiliano kwa ajili ya
kurahisisha maisha.
No comments:
Post a Comment