
Meneja wa Utawala na Rasilimali
Watu wa Mamlaka ya Maji Kahama na(Kashwasa), Denis Mlingwa akimuonyesha
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi, Charles Kitwanga (kushoto) sehemu ya kuchukulia dawa ya Kituo
kipya cha Afya cha Ihelele jimboni humo kinachotarajiwa kufunguliwa hivi
karibuni kiweze kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo. Kituo hicho
kitaongozwa na Kashwasa wakishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya
Misungwi. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (aliyevaa koti) akishangiliwa na mamia ya wananchi wa Kata ya
Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa
ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao.
Waziri Kitwanga ameanza ziara jimboni humo leo. Picha zote na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (aliyevaa koti) akicheza ngoma ya Kisukuma iitwayo Wachwechi
wakati alipofanya ziara katika Kijiji cha Lutalutale, Kata ya Mbarika
jimboni humo. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbarika jimboni humo wakati
kiongozi huyo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na
kuzungumza na wananchi katika kata hiyo. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (kushoto) akimkabidhi mpira wa miguu Mwakilishi wa Kitongoji
cha Kashishi, Kata ya Sumbugu, Lucas Chai. Mbunge huyo alitoa mipira ya
miguu katika kata mbalimbali jimboni mwake. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment