KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 4, 2016

ATLETICO MADRID YATINGA FAINALI ULAYA

Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munchen ya Ujerumani. Wakiwa na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza nchini Hispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Xabi Alonso.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak aliokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya mshambuliaji Antoine Griezmann kusawazisha na kuwa 1-1
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi ya mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres kuokolewa na mlinda mlango Manuel Neuer.
Kwa maana hiyo Atletico watakutana katika fainali mjini Milan tarehe 28 Mei na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu

No comments:

Post a Comment