KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 1, 2016

GEORGE WEAH ATANGAZA TENA NIA YA URAIS LIBERIA

Close up of Mr Weah's face as he speaks into a microphone
Mchezaji wa kimataifa wa zamani wa Liberia George Weah atagombea tena urais kwa mara pili.

Alisema anayo maono ya kuibadili nchi yake.

Bw. Weah ambaye alichezea timu mbalimbali kama vile Paris Saint-Germain, AC Milan na  Chelsea, ni miongoni mwa wachezaji wa Kiafrika mbao wako juu viwango vya Fifa  kwa karne ya 20.

Jaribio lake la kwanza la kuingia Ikulu liligonga mwamba baada ya kuangushwa na Rais wa sasa Bi.  Ellen Johnson Sirleaf.

Muhuma wa pili wa Rais wa sasa unamalizika mwaka 2017 na kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo hawezi tena kuombea nafasi hiyo.

Wakati akisakata kabumbu , Weah alikuwa balozi wa hiari wa UN na baadaye alihamia kwenye siasa. Kwa sasa ni Seneta wa Jimbo la Mashariki la Montserrado, ambalo linajumuisha mji Mkuu wa  Monrovia.

Mwaka 2011 aligombea U-Makamu wa Rais Chini ya Winston Tubman lakini hawakufua dafu.

Bw.Weah anatoka chama cha upinzani cha Congress for Democratic Change (CDC) party.

Akitangaza nia hivi karibuni mjini Monrovia, Weah alisema alisema amekuwa 'muhanga' wa umasikini kama walivyo wafuasi wake na kwamba ataanzisha mafunzo ya ufunsi stadi.

No comments:

Post a Comment